Rayvanny humiliates Harmonize for preying on his step daughter

0
222
Rayvanny humiliates Harmonize for preying on his step daughter

By Rayvanny via FB

Dunia inamaajabu yake lakini sijawahi ona mtu wa ajabu kama wewe my bro @harmonize_tz Ni binadamu wa aina gani wewe ambae unataka kua na mama na mtoto pia tena kwa nguvu zote na unatuma hadi utupu wako bila hata kuogopa nafasi ulionayo kwenye jamii kujidhalilisha kua kama ulivyozaliwa na angali wewe ni kioo cha jamii.

Ni roho ya ajabu sana ulionayo yani KILA NIKIKUWAZA SIPATI JIBU NDUGU YANGU. Ulikua unawapigia simu viongozi mbalimbali juu ya swala langu mimi sasa nawaza leo hii utawaangaliaje ??

Wewe ni balozi wa kampuni na zimekupa heshima kama balozi sasa nawaza unapata wapi ujasiri wa kutuma utupu wako ni kampuni gani inakubali fedheha hii na je wanakuonaje kwa kitendo hiki ulichokifanya kinachodhalilisha wanawake hasa mama ?

Hivi hukumfikiria mama ambae aliekupa heshima wewe na kukuweka karibu na kukutambulisha familia yake ? Yani unataka ukatembee na mwanae wa damu yani mwanae wakumzaa? LEO HII MWANAO WAKIKE AKIKUA AKASIKIA UCHAFU HUU ANAKUONA NI BABA WA NAMNA GANI WEWE UNAEMTAKA MAMA NA MTOTO ?

USHAURI WANGU: OMBA RADHI KWA WAZAZI NA KINA MAMA NIKIWA NA MAANA WANAWAKE AMBAO NI MAMA ZETU WANASTAHILI HESHIMA SIO KUDHALILISHWA KAMA ULIVYO FANYA WEWE NA UNAIGIZA KAMA HAKIJATOKEA KITU….. UKIHESHIMIWA BASI JIHESHIMU

Rayvanny humiliates Harmonize for preying on his step daughter

Source: KENYAGIST.COM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.